Mbunge wa Viti Maalum,kupitia UVCCM (CCM) mkoani Arusha Bi. Catherine Magige ambaye ni Kiongozi
wa Taasisi ya Catherine Foundation, akimkabidhi
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida Mokit msaada wa
mablang’eti ya kujifunikia wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.
Taasisi ya Maendeleo isiyo ya kiserikali ya Catherine
Foundation ya jijini Arusha Machi,28,2013 imetoa misaada mbalimbali ya vyakula
kwa wagonjwa Hospitali ya Mt Meru na vituo viwili vya Yatima vya Faraja na
Lohada Moshono vyote vya jijini humo.
Mbunge wa Viti Maalum wa UVCCM (CCM), Catherine Magige ambaye
ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa
Hospitali ya Mt. Meru ya jijini Arusha na kuwapa zawadi mbalimbali.
Misaada hiyo ya vyakula na sabuni pamoja na kuwatembelea
wagonjwa kufanyika ikiwa ni sehemu ya kuwapa faraja wagonjwa na yatima hao wakati
huu wa kuelekea sikukuu ya Pasaka ili nawao wajisikie ni miongoni mwa jamii.
No comments:
Post a Comment