Thursday, February 7, 2013

USAFI JIJI LA ARUSHA NI CHANGAMOTO KUBWA IWAPO USIMAMIZI WAKE HAUTASIMAMIWA SAWASAWA

MKUU WA MKOA WA ARUSHA MHE. MAGESA MULONGO SIKU YA UZINDUZI WA RC USAFI DAY TAREHE 01/02/2013

HAFANYAKAZI WA HALMASHAURI YA JIJI WAKISAFISHA MTARO YA MAJI MACHAFU YA MVUA BILA KUJALI TAKA HIZO ZINAENDA WAPI LEO SAA 08.24.
Na Mwandishi wetu
Kampeni aliyozindua Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Magesa Mulongo tarehe 01 Februari,2013 la kuhakikisha jiji linakuwa safi halitafanikiwa iwapo sisi washika dau pamoja na taasisi inayosimamia kazi hiyo kwa karibu ufanisi wao utakuwa siyo wa dhati na makini. 

Mwanahabari wetu alifanikiwa kuona jinsi ya baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha waliokuwa wanasafisha mtaro, bila ya kuhakikisha kuwa taka na mlundikano wa udongo unaotolewa kwenye mtaro unahamishwa au kupelekwa kunakohusika na kuamua kusambaza barabarani, katika Kata ya Kaloleni Mtaa wa Ethiopia mkabala na  Hoteli ya Kitalii ya Briston.

Tunaiomba Halmashauri ya Jiji la Arusha, kuwa makini katika kuhakikisha kuwa kero kama hizi hazijitokezi, kwani mvua mvua ikinyesha taka na udongo huo unarudi ulikotolewa, na hii ni kero kwa jamii na wananchi kwa ujumla.Halmashauri imsaidieaidia Mkuu wa Mkoa kuhakikisha kuwa usafi unafanyika inavyotakiwa ikiwa kama ni sehemu yao.

No comments:

Post a Comment