Monday, April 15, 2013

Meja Jenerali Makame afariki dunia

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhBTJyTsy4u-hZdNa-qRla85ctK3Kw0k4_EYuz2N7-G3VWGjpQ3cpeQlYPIDqEVQZQ8A2hAXyZ418xISbEcALjNIuAaGZ0ErklUucw8dds_YVr98iw8ZU0zCpDRZ4oABPZVYhNC9zt3ps6v/s1600/01+(2).jpg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhdmcQQcIt-G-_cFJE6DIC46bPAZEPWkZ3xwZGnc6vw_a_m4-2itqYxBSPX9VAtWJfRsqIj7GkvoGVxzOR8AyVXSLV38rrWnwzuFI9-TIAuEOFYCnOqWD_aHUAZNztzS5-wKasDmJKMABZe/s1600/9+(1).jpg

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin William Mkapa akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam.

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjP7ZM3xWDy-QVsXFuJnpFRCLh6XROGeLnhLl4aIvNyoto87_Uj9_rbjxK_i1s2ZCXxFbEELUbYZKtXXzobXXPtchs825FYttCLfUC5w_Db1JVThB9t1fy9_VhLWpZiLonQIHONl5J7rMKM/s1600/11+(1).jpg

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davies Mwamunyange akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhKqgmcIB318k3rjvZ8bD4hT0tX7oW8M365wwrLr_OhKajw70vv3cK4nOBvKunZaN45VQltTMXwV5DoyPAty5k3ieLNQ2_IcuStdfQ9zjyydj50it518LqJSpkhhxOkPk-UWB-EcnjAU9bU/s1600/5+(3).jpg

Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJ9PMIIMn_zUa9nEaCONKK7Oui84X5SjjLqyUxTRsPq2E0n_0cbveAbNrKDB0Zi91fTAYexBL1MM6MCwjT6rSLFeVGX-KzYJLRNSPXFsIgKeFLv3ccaSoIarzzoRRvCBeppEsiMLf9skYU/s1600/4+(5).jpg

Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj99iMzdSRJCXZ_utYixBgJ4HL4vX_IygCGQRbSiVPaltGGO7I2WyXqIyqWB04k7m8BsN45xQoy7j-n49anlWs5DG7k0HqqGZWi3-wup71LjnMCv9oNSgTJbhG5GVzcXWs7j-ypIvhprGLL/s1600/6+(3).jpg

Jeneza likiwekwa sehemu maalum kwa ajili ya heshima za mwisho.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnl9B-3gsg-WrymLLS3vOOAVA8FWH-7NmMTgGVA0lhs2f9t5YnXOVTFlNcJR6Bbaqh0E2UBuYNODXrGpLli2CZ0iWmMrGrYJ0S01gqjMXebzafD10J8MFBsOp0SGnUc84TyEth3Z6OQ8aK/s1600/2+(5).jpg

Makamu wa Rais Dkt. Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Mkuu wa Majeshi Davis Mwamunyange.

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgNE0XisRDaeDbtJTbdOKhtGNJqKx1FcDiW8G6m7e2WVMx25KQcvKJSOJkjfitoyqXtb9QHGb6IuyJ7yezxq_spbyAx7Y690CEEMVm0pVHLpC9-WSWon44GkrjCMLEEIeqrRzEcTxOfFt1w/s1600/1+(3).jpg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjquk4CSmaHpZ4Yw2UPKvaf0T2h7ttfBS5MGJU5P_FaIwevwSEj0PASGCJ10bRWzD-8laAvmrwGhcEzYwxx6P-lk31wuRtcCQuQCs0oeelW3YyHSc6-OZEgqlw_9hUpU4ilNZYv2HjGi83v/s1600/10+(1).jpg

Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akitoa mkono wa pole kwa ndugu wa Marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam.

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjNYH0Mg01es6ABrUkuoG-D3SnXQAR3CSNY6XnnKiSCUhHoRn1hmndIOCdeR-3PZGaQ_VezPMQomSUouPrFhzQ0uUSUeuahS6F29tknAwqJ3y_vRuCFfxO3n4DgTMDLN9VRf-NV_nBLdoLb/s1600/3+(5).jpg

Toka kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ),Luteni Jenerali,Samuel Ndomba,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,IGP Said Mwema na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,Kamishna Jenerali John Minja wakiwa kwenye msiba wa Marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam.

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhulkSYpBPfgzhwaRTdkIjPWGf4uSPpQpo06JzsmyK3c2hV6Uytqv77rbBTsxZxogqWez75NY-zLcZE6JnA1zLEqDfHpSwNrqKMUDCKT9GaP3i9TofzNM3igUpyCOlYPP8wX9nyEHrFhJYV/s1600/8+(2).jpg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa mkono wa pole kwa ndugu wa Marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYcm_uYQE3TImM5Zxm4zrN8DihanQw4PayDAVero_CtOPPvBwsgC5yClsEnjtvHnFz7E8Qwd1S2whDoLbUms0LJ8qv7C31s9gIhivnMd0PyKuT9S5NDcaQNqIsyNquzfB3uBMHRx97i26X/s1600/12+(1).jpg

Ndugu wa Marehemu wakiwa wakiwa katika majonzi na huzuni kubwa baada ya kuondokewa na Mpendwa wao.Picha na OMR.

ALIYEKUWA Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali mstaafu Rashid Makame amefariki dunia. Meja Jenerali Makame aliaga dunia jana alfajiri katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam, alipokuwa amelazwa. Enzi za uhai wake, mbali na kuwa mkuu wa JKT, Meja Jenerali Makame pia aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Balozi wa Tanzania nchini Malawi.


Taarifa za kifo hicho zilitolewa jana kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) makao makuu.

Taarifa hiyo, haikufafanua Meja Jenerali Makame alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani, hadi kufikia hatua ya kulazwa hospitalini hapo.

Historia inaonyesha, Meja Jenerali Makame alijiunga na JKT kwa kujitolea mwaka 1963 katika Kambi ya Mgulani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Makame alipitia kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi na hivyo kuwa kiongozi wa kujitolea.

Alijiendeleza kielimu kwa kozi mbalimbali za kijeshi hadi kufikia cheo cha Senior Master, kabla ya JKT kuunganishwa na JWTZ mwaka 1975.

Baada ya majeshi hayo kuunganishwa, mwaka huo huo marehemu alipewa cheo cha Meja.

Alishika madaraka mbalimbali ya uongozi, yakiwamo ya seksheni, platuni, kombania, mkuu wa kikosi na Idara ya Mafunzo na Utendaji Kivita makao makuu ya JKT.

Kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa JKT, marehemu alipandishwa vyeo mbalimbali hadi kufikia cheo cha Meja Jenerali. Aliteuliwa rasmi kuwa mkuu wa JKT mwaka 1989 hadi 2001 alipostafu.

Akiwa mkuu wa jeshi hilo, aliweza kuboresha sekta ya michezo, sanaa, utamaduni, ukamilishaji wa nyumba ya kisasa ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kijijini Butiama.

Mwaka 2004, Rais mstaafu Benjamin Mkapa alimteua kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwake Mikocheni, karibu na Msasani kwa Mwalimu Julius Nyerere.

No comments:

Post a Comment