Wednesday, January 30, 2013

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AELEZA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI KWA KIPINDI CHA MWAKA 2005-2012


.. 9
 Mkuu wa Wilaya ya Arusha akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na utekelezaji wa ilayani ya uchaguzi kwa kipindi cha mwaka 2005-2012

Imeelezwa kuwa ilani ya CCM kwa miaka saba katika Wilaya ya Arusha imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika njanja zote zikiwemo sector ya Elimu ,Afya,Mazingira,na Miundombinu ikiwemo Mji wa Arusha kuwa Jiji rasmi.

Hayo yameelezwa na mkuu wa ilaya ya Arusha John Mongella mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa hiyo katika hotel ya palace hapa jijini arusha  na kusema kuwa sector zote zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani toka mwaka 2005 hadi mwaka 2012 karibu utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi imetekelezwa.

Bw Mogella amesema katika sector ya elimu amesema wamejenga madarasa 172,matundu ya vyoo 225,ambapo Shule za Msingi zimeongezeka 70 ambapo kwa Shule za Sekondari zimeongezeka 23ambapo awali zilikuwa saba ,ambapo walimu na vifaa vya usimamizi wameongezeka 534 kwa miaka hiyo saba pamoja na idadi ya vyuo vya shahada ya juu vikuu kupandishwa hadhi  na kufikia 8 .

Amesema kwa upande wa afya Mkuu Mongela amesema kuwa wameweza kuboresha huduma ya mama na mtoto ambapo vituo 5 na zahanati 68 zimeboreshwa kwa uhakika wa upatikanaji wa dawa na huduma bora,huku akifafanua kuwa wameipandisha hadhi kituo cha afya cha kanisa st.elizabert na kuwa hospitali ya wilaya huku akisema kuwa katika hospitali hilo kuna kituo kikuu kitakachotoa huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi ambapo kitatoa huduma bure.

Kwa upande wa miundo mbinu amesema kuwa barabara nyingi zimejengwa katika kiwango cha lami katika barabara hasa za katikati ya mji ambapo hadi sasa barabara 23 zenye urefu wa km 8 zimekamilika ambapo mradi huu unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kiasi cha dola million 7 za kimarekani,ambapo  awamu ya kwanza na awamu ya pili itajenga barabara ya Njiro,Kanali Ndomba,pamoja na kujenga dampo la kisasa ,yakiwemo ujenzi wa madaraja 9 katika Wilaya ya Arusha.

Mongela akiongezea kuhusu upande wa mazingira hasa upande wa maji amesema asilimia 83 ya wakazi wanaoishi katika Jiji la Arusha wanapata maji safi na salama tofauti na awali ilikuwa ni asilimia 42 tu ya wakazi ndio waliopata huduma hiyo ya maji salama ,ambapo amesema kuwa wanamkakati wa mradi wa ujenzi wa miundo mbinu utakao gharimu shilingi million moja.

Katika swala la mazingira amesema wamepiga hatua kwani wameweza kulinda vyanzo vya maji kwa kushirikiana na AUWSA ikiwemo misitu,kuzuia uoshaji wa magari pembezoni mwa mito,na kuzuia ukataji wa miti katika misitu iliyopo ndani ya Jiji ikiwemo kuboresha usafi ndani ya Jiji letu.

Aidha alisema pamoja na mafanikio hayo pia kuna changamoto zinazoikabili Jiji hili ikiwemo ya kusafisha hati chafu ya jiji hili ,ambapo baadhi ya viongozi wabadhirifu wa raslimali wamewajibishwa kutokana na makosa yao ikiwemo kufikishwa mahakamani pamoja na kufukuzwa kazi.

Pia aliongezea kuwa changamoto nyingine ni Demokrasia ambapo Wilaya yetu ina viongozi wa vyama  vya siasa tofauti, tofauti ambapo alitolea mfano Mbunge wa Chadema katika jimbo la mjini Arusha kutofautiana katika utekelezaji na uwajibikaji katika kuwatumikia 
wananchi wa Wilaya hii .

Mwisho Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mongella alitoa wito kwa wakazi wa Jiji la Arusha kuendelea kushirikiana na viongozi katika kuhakikisha hali ya jiji inakuwa tulivu ambapo kwa kiasi kikubwa katika swala la ulinzi na usalama ikiwemo dhana ya ulinzi shirikishi 
na kutii sheria bila shuruti.

Na Woinde Shizza,Arusha

No comments:

Post a Comment