Thursday, January 17, 2013

Waziri aipa masaa 24 meli yenye dizeli chafu kuondoka nchini

Written by  Mwandishi wetu
Waziri wa Uchukuzi Dk Harison  Mwakyembe

Waziri wa Uchukuzi Dk Harison  Mwakyembe amipa masaa 24 meli iliyokuwa imeleta kuuza mafuta aina ya dizel kuondoka mara moja nchini baada ya kubaini kuwa mafuta iliyoleta hayana ubora wa viwango.

Akiwapongeza maafisa wa TBS nchini kwa kubaini uozo huo na kisha kuweka mbele msalahi ya taifa hili Dk Mwakyembe mbali na kuitimua Meli hiyo yenye namba za usajili IMO 9381732 ameahidi kuwafungulia mashtaka wale wote wanaohusika na meli hiyo.

Dk Mwakyembe amewaambia waandishi wa habari kuwa mwezi disemba meli hiyo iliingiza bidhaa hiyo mbovu nchini lakini maafisa wa TBS walishtukia na kuiamuru iondoke lakini cha kushangaza iliondoka na kukaa siku tisa kisha kurudi tena nchini kuuza hayo hayo mafuta.

"Tanzania si kichwa cha mwenda wazimu, na hatuwezi kuwa jalala la bidha feki na zisizokidhi  viwango vya ubora, nawapongeza maafisa wa TBS kwa kuonyesha uzalendo, nazidi kusisitiza kuwa afisa asiyewajibika ipasavyo katika eneo lake atawajibishwa tu,"alisema Dk Mwakyembe.

Alisema uhuni waliokuwa wanataka kufanya wamiliki wa meli hiyo hautakiwi kuungwa mkono hata kidogo, kwani dizeli hiyo isiyo bora ingeweza kuhatarishwa kwa kiasi kikubwa mitambo ya uzalisha hapa nchini.

No comments:

Post a Comment