Saturday, January 26, 2013

WATALII 100 KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari  jijini Arusha. 
Mkurugenzi wa Wings of Kilimanjaro Australia
Paula Mcrae  ambaye ni Meneja mradi akiongea na wanahabari
Watalii zaidi ya 100 kutoka nchi 25 ulimwengu wanatarajiwa kupanda mlima kilimanjaro kwa miguu hadi  kilele cha uhuru ambacho ndicho kilele cha juu katika bara la Afrika   sanjari na kuruka na miamvyuli maalum wakiwa juu ya kilele cha mlima huo hadi chini

Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari  jijini Arusha  alisema kuwa zoezi hilo limeandaliwa na TANAPA kwa kushirikiana na Taasisi ya Wings of Kilimanjaro iliyopo nchini Australia ambapo ni mara ya kwaza kufanyika Tanzania

Shelutete alisema kuwa wageni hao zaidi ya 100 wanatoka nchi 25 ulimwenguni hivyo watapanda mlima huo pamoja na kutua chini wakiwa na miavyuli maalum katika viwanja vya shule ya sekondari ya Mweka ya umbwe,na chuo cha ufundi cha mweka

“Wataruka na vyombo hivyo kuanzia tareh 5-6 februari  2013 na kutua katika maeneo ya umbwe na kibosho,, kulingana na hali ya hewa itakavyo kuwa ,,hali ya mlimani haitabiriki unaweza kukuta ukungu hivyo kuwafanya wasione chochote “alisema Shelutete

Pia aliongeza kuwa zoezi hilo linaonyesha namna gani mlima huo wa Kilimanjaro umekuwa na manufaa katika eneo la kiuchumi kwa watanzania huku akisema kuwa zoezi hilo litahusisha pia katika uchangishaji wa fedha kiasi cha dola milioni moja za kimarekani ambazo zitabaki hapa hapa nchini kupitia mashirika yasiyokuwa yakiserikali ya Plant with purpose,One Foundation,WorldServe Internation

“Fedha hizo zitatumika kuwasaidia watu wanaoishi kuzunguka mlima huo kwa kuchimba visima vya kuwapatia maji safi,zoezi la kupanda miti itakayo saidia kutunza mazingira,kuwasidia jamii yenye uhitaji kuonokana na umaskini pamoja kuangalia namna gani wataweza kuondokana na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi”alisema

Hata hivyo alisema kuwa faida watakayopata wananchi wa Kilimanjaro ni pamoja na zaidi ya ajira 600 kupatikana kutokana na zoezi hilo ambapo wapishi watahitajika,wabeba mizigo na waongoza wageni

Pia zoezi hilo pia linaratibiwa na kampuni ya Top of Africa iliyopo mjini Moshi.

No comments:

Post a Comment