Mshambuliaji wa Arsenal,Theo Walcott (kulia) akimuangalia kipa wa Reading,Adam Federick (kushoto) akipangua mpira wakati wa mechi ya kombe la Capital juzi kwenye Uwanja wa Madejski,Mjini Reading. |
Tulilazimika kuwaonyesha kwamba tunaweza kufanya vizuri, hatukukata tamaa, ilikuwa siku yetu."
LONDON, England
Theo Walcott alifunga 'hat trick' na kuiwezesha Arsenal iliyokuwa nyuma kwa mabao 4-0 kuibuka na ushindi usiotarajiwa wa mabao 7-5 dhidi ya Reading katika mchezo wa dakika 120 Kombe la Capital.
Mshambuliaji, Marouane Chamakh naye alifunga mara mbili katika dakika ya 102 na 120 kwenye Uwanja wa Madejski.
Mabao ya Walcott yalikuja katika dakika za 45,90 na 120.
Mabao ya Reading yalifungwa na Roberts dakika ya 12, huku Koscielny akijifunga mwenyewe
katika harakati ya kuokoa goli dakika ya 18, Leigertwood dakika ya 20, Hunt dakika ya 37 na Pogrebnyak dakika ya 116.
Reading walikuwa mbele kwa mabao 3-0 ndani ya dakika 20 za mwanzo wa mchezo, kabla ya Noel Hunt kufunga bao la nne.
Matumaini kwa Arsenal yalirejea kabla ya mapumziko baada ya Walcott kufunga bao la
kwanza na kutengeneza pande lililozaa bao la pili.
Olivier Giroud na Laurent Koscielny walifunga na kufanya matokeo kuwa 4-3, kabla ya Walcott
kufunga bao la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 4-4.
Chamakh na Pavel Pogrebnyak walifunga mabao katika muda wa nyongeza, kabla ya Walcott na Chamakh kufunga baadaye.
"Yalikuwa matokeo ambayo hayakutegemewa,' alisema Walcott wakati akiongea na Sky Sports.
"Tulianza taratibu, ilitulazimu kuamka. Kocha alituambia hakuna namna ni lazima tushinde mchezo. Hii haikuwa Arsenal nayoifahamu.
Tulilazimika kuwaonyesha kwamba tunaweza kufanya vizuri, hatukukata tamaa, ilikuwa siku yetu."
"Tulionyesha uwezo wetu, kuna wachezaji wengi vijana walicheza na hii imewapa uzoefu mkubwa. Nadhani itawasaidia kwenye mechi za Ligi Kuu
"Tumefunga mabao saba ugenini. Safu ya ushambuliaji ilicheza vizuri.'
Kocha Arsene Wenger akimwongelea Walcott, alisema hakuna mchezaji anayecheza Arsenal akaonyesha hali ya kukata tamaa.
"Unaweza kuwa mshindi wa kihistoria nikiwa hapa Arsenal," alisema Wenger.

No comments:
Post a Comment