Thursday, January 3, 2013

VIJANA WA CCM ARUSHA WAFUNDWA

DSCF1813
Add caption
Mwenyekiti wa  (CCM)  Mkoa wa Arusha,
Ndg.
Onesmo ole Nangole

VIJANA wa chama cha mapinduzi mkoani Arusha wametakiwakuungana na kuwa kitu kimoja huku wakiepukana na makundi na  kuhakikisha kuwa wanarudisha heshima ya chama hicho pamoja na kutekeleza  ilani ya chama .

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa  (UVCCM)  mkoa wa Arusha, Nangole wakati  akizungumza na umoja wa vijana mkoani wa Arusha (UVCCM) katika kikao kilichofanyika katika hotel ya golden rose iliyopo mjini hapa.

Alisema kuwa, uchaguzi umeisha katika maeneo mbalimbali hivyo kilichobakia hivi sasa ni kuungana na kuwa kitu kimoja huku wakivunja makundi mbalimbali na kuweza kujipanga upya na kuweza kurudisha heshima ya chama hicho mkoani Arusha

Aliongeza kuwa, mgawanyiko ulipo ndani ya chama hicho ndio unawapa wapinzani nafasi ,hivyo umefika wakati sasa wa kuamka na kusimama katika nfasi zao kama vijana wenye nguvu  huku wakipeperesha bendera ya chama hicho na kuhakikisha wanajipanga ipasavyo kwa kipindi kijacho.

‘Nyie wenyewe mnajua kabisa kipindi cha uchanguzi jamani tulitukanwa sana na wapinzani wetu na walitudhalilisha sana ,na kutuonea pia kuna kipindi tulipita wilaya  ya Arumeru  katika eneo la Usa –River tukiwa tumefuatana na Rais mstaafu awamu ya tatu, William Mkapa tulishangaa kusikia mayowe eti vijana wakiona  bendera ya CCM wanapiga mayowe hicho kitu kiliniuma sana laikini pamoja na hayo yote bado hatujachelewa tuna muda wa kujipanga upya ‘alisema Nangole.

Alisema kuwa, umefika wakati sasa wa vijana mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanajipanga ipasavyo na kwa kushirikiana ili kuona mkoa huo unaendelea mbele na hakuna majungu yoyote miongoni mwao.

Aliwataka vijana hao kudumisha umoja na kufanya shughuli za chama hicho kwa  ushirikiano  kwani  wasipokuwa na umoja, ni wazi kuwa  nguvu ya chama hicho itakuwa kidogo sana ,hivyo ni wajibu wao  sasa kutumia nafasi zao kama vijana na kurudisha heshima ya chama hicho kwa kasi kubwa na ilivyo kuwa hapo awali.

Aliutaka umoja huo kukaa pamoja na kufanya vikao mbalimbali kuanzia ngazi za serikali za mitaa, wakishirikiana na madiwani pamoja na wabunge na kuhakikisha kuwa wanatekeleza ilani ya uchaguzi kwani ifikapo mwaka 2015 wananchi watauliza walichotekelezewa.

‘Kila kijana mkoa wa Arusha ajiandae sasa  kumekucha , baada ya sikukuu za krismas tunaanza mikutano na kuzunguka kila kata na kijiji mkoa wa Arusha na mkutano huo utalenga kurudisha heshima ya chama chetu pamoja na kukiboresha chama na vijana ndio wenye jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa chama kimeimarika na kurudia katika hali ya zamani na kuendelea kupendwa na kila mmoja’alisema Nangole.

          

No comments:

Post a Comment