Sherehe za kutangaza vivutio vya
asili vya bara la Afrika zinategemea kufanyika katika hoteli ya Mt Meru katika
jiji la Arusha Tanzania
tarehe 11 February 2013 kuanzia saa nane mchana.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi
ya Utalii Tanzania
viongozi mbali mbali wa kitaifa na kimataifa ambazo wanatarajiwa kuhudhuria
sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Mizengo Pinda. Rais wa Taasisi iliyoendesha shindano hilo la kutafuta Maajabu hayo Saba la Seven Natural Wonder
Dr Philip Imler kutoka Marekani anatarajiwa kuwasili tarehe 9/2/2013 tayari
kabisa kutangaza vivutio Saba vya Asili vya
bara la Afrika.
Tanzania ilikuwa na vivutio vitatu
vilivyoingia kwenye kinyanganyiro hicho ambavyo ni Mlima wa Kilimanjaro, Bonde
la Ngorongoro na wanyama wanaohama wa Seregeti. Tanzania
imekwisha tajwa kuwa miongoni mwa washindi ambao angalau kivutio kimoja ama
zaidi Saba ya Asili Afrika.
Macho na masikio ya watanzania ni
kujua ni kivutio au vivutio gani hivyo vya Tanzania vimeweza kushinda.
By. Geofrey Tengeneza
No comments:
Post a Comment