Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha
(ACP) Liberatus Sabas akiwaonyesha waaandishi wa habari (hawapo pichani) madawa
ya kulevya aina ya bangi yaliyokuwa kwenye moja ya viroba kati ya 20
vilivyokamatwa na Polisi,mkoa Arusha.
MNAMO TAREHE 31/01/2013 MUDA WA
SAA 7:30 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA LOSOITI KIJIJI CHA KIMOKUWA WILAYANI
LONGIDO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKISHIRIKIANA NA ASKARI MGAMBO WALIFANIKIWA
KUMKAMATA MTU MMOJA AITWAYE MANDEGE S/O PAKASI (54) MFUGAJI NA NI MKAZI WA
KITONGOJI CHA LOSOITI AKIWA NA MAGUNIA 20 YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI
YANAYOKADIRIWA KUWA NA UZITO WA KILOGRAMU 50 KILA MOJA.
TUKIO HILO LILITOKEA MARA BAAADA
YA ASKARI HAO KUPATA TAARIFA TOKA KWA RAIA WEMA, AMBAPO INAELEZWA KWAMBA
MTUHUMIWA HUYO PAMOJA NA WENZAKE WAWILI WALIKUWA WANASAFIRISHA MADAWA HAYO KWA
KUTUMIA WANYAMA AINA YA PUNDA AMBAO WALIKUWA KUMI AMBAPO KILA MMOJA ALIKUWA
AMEBEBESHWA MAGUNIA MAWILI.
MARA BAADA YA WATU HAO KUWAONA
ASKARI HAO WATUHUMIWA WAWILI WALIKIMBIA NA WAKAFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA
MMOJA.
JESHI LA POLISI MKOANI HAPA BADO
LINAENDELEA KUMHOJI MTUHUMIWA HUYO HUKU WATUHUMIWA WAWILI WALIOKIMBIA
WANAENDELEA KUTAFUTWA. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI
MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI,
(ACP) LIBERATUS SABAS
No comments:
Post a Comment