.jpg)

Na Mahmoud Ahmad,Arusha
TANZANIA imepata tuzo tatu za
maajabu saba ya Afrika kupitia vivutio vyake bora vya utalii vya Mlima Kilimanjaro,Hifadhi ya Ngorongoro na
Hifadhi ya Serengeti ambayo ndio iliongoza kwa kupata kura nyingi kuliko nchi
nyingine yeyote.
Akitangaza matokeo hayo jana
mjini hapa rais wa taasisi iliyoandaa
tuzo hiyo Dk. Phillip Imler wa Marekani mbele ya waziri mkuu Mizengo Pinda
alisema sababu iliyopelekea Tanzania kupata ushindi huo ni kutokana na kuwa na vivutio vya kipekee.
Akielezea hifadhi ya taifa ya
Serengeti alisema kuwa ndio hifadhi ya kipekee iliyopata kura nyingi na
kutokana na tabia za misafara ya wanyama wanaohama kwa msimu maarufu kama annul animal migration.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda,
aliyekuwa mgeni rasmi katika ghafla hiyo, alisema kuwa nchi za Afrika zina
vivutio vingi vya utalii na fursa kubwa ya kukuza pato kupitia utalii huo.
Alisema kutokana na sifa ambayo
Tanzania
imezipata kupitia vivutio vyake vitatu itaendelea kuvitunza kuhakikisha
kuwa vinavutia zaidi watalii na kuongeza
pato la taifa.
“Afrika ina vivutio vingi vyenye kuvutia hivyo kila nchi ni lazima
ijivunie rasilimali hizo kwa kuvitunza na kuviendeleza,”alisema
“Kwa Tanzania ni bahati ya
pekee kwa kuweza kupata tuzo tatu za maajabu saba ya Afrika ambazo ni za Mlima Kilimanjaro, Bonde la
Ngorongoro pamoja na hifadhi ya Taifa ya Serengeti hivyo ni wajibu wa kuvitunza
na kuviendeleza,”alisema Pinda.
Aliongezea kuwa iwapo watanzania wataendeleza tabia ya
utunzaji wa vivutio vilivyopo nchini, nchi itaendelea kupata sifa duniani kote.
Naye Mkurugenzi wa Hifadhi za
Taifa,(TANAPA),Dkt. Alan Kijazi alisema
mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu barani Afrika na hivyo una kila sababu ya
kushinda na watanzania waendelee kuutunza.
Dkt Kijazi alisema kuwa hifadhi
hiyo imeshinda kwa kuwa kuwa na wanyama wa kila aina kama Big Seven, Simba,
tembo, Viboko, Nyati, Vifaru, Sokwe na Mamba.
Mbali na Tanzania Dk.Imler
alivitaja vivutio vingine vilivyoshinda kuwa ni Red sea Reefs, Okavango
Inland delta iliyopo nchini Botwasana, Sahara Desert
na River Nile.
Aidha Waziri wa Maliasili na
Utalii, Balozi Khamis Kagasheki alisema ushindi huo ni historia kubwa duniani
na kwamba ni jambo la watanzania wote kujivunia.
Pia aliwashukuru wananchi
walioshiriki katika mchakato mzima wa kupiga kura na kuviwezesha kuingia katika
ushindi kwa mara tatu.
No comments:
Post a Comment