Saturday, February 16, 2013

NBC YADHAMINI HAFLA YA MFUKO WA NSSF MJINI ARUSHA






Waziri wa Kazi na Ajira, Gaundencia Kabaka (kulia) akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Uwekezaji wa Benki ya NBC, Minnie Adolf Kibuta katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa washiriki wa mkutano wa tatu wa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha . Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF, Aboubakar Rajab.
 
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaundencia Kabaka (katikati) akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki ya NBC kwa washiriki wa mkutano wa tatu wa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
 
 Msanii wa muzii wa izazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond’ akikonga nyoyo za wadau wa NSSF katika mkutano huo jijini Arusha. https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhBVjVaW4l1NYVDudcwcOPI6H1QDC3sKkfL2OLYNzMliMrQxWEiefeoPCLerEbsQd2pLbeFNV-R-I9NEWG4opnSLYht-CHNTPaaMrIf32Msm6sRZeg8T1HqyOjaTH328gey8smIREEj2bDt/s1600/05.JPG
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF), Crescentius Magori (kulia) akizungumza na  Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Uwekezaji wa Benki ya NBC, Minnie Adolf Kibuta katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa washiriki wa mkutano wa tatu wa Wadau wa NSSF kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
 
  Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Uwekezaji wa Benki ya NBC, Minnie Adolf Kibuta (katikati) akipozi kwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NBC katika hafla hiyo jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment