Sunday, January 20, 2013

Mpasuko Moravian, Mch Fumbo ajirudisha madarakani

Written by  Mwandishi wetu
Mchungaji Clement Fumbo akitangaza uongozi mpya wa mpito utakaoliongoza jimbo kwa mwaka mmoja hadi kikao cha sinodi kitakachofanyika mwaka 2014

Mpasuko mkubwa umeliandama kanisa la Moravian Jimbo la Mashariki kufuatia Mwenyekiti aliyesimamishwa MchuMchungaji Clement Fumbo akitangaza uongozi mpya wa mpito utakaoliongoza jimbo kwa mwaka mmoja hadi kikao cha sinodi kitakachofanyika mwaka 2014ngaji Clement Fumbo kutangaza uongozi mpya wa mpito wa jimbo hilo utakaodumu kwa muda wa mwaka mmoja 2013-2014, waka uongozi wa jimbo unaojulika na kanisa kuwepo madarakani

Akitangaza leo jijini Dar es Salaam Mch. Fumbo alisema baada ya kipindi kirefu cha mgogoro ndani ya kanisa uliotokana na jaribio la mpango wa mapinduzi ya kumpindua na kumuondoa yeye madarakani kushindwa ameamua kuunda Halmashauri mpya ndani ya kanisa.

Awali mwaka jana katika kikao cha Sinodi kilichohudhuriwa na wachungaji mbalimbali wa kanisa la Moravian jimbo la Mashariki iliamuriwa mch.Fumbo apumzike madaraka yake hadi uchaguzi wa sinodi utakaofanyika mwaka 2014.

Aidha sinodi hiyo ilimpatia mamlaka yote makamu mwenyekiti wa jimbo Sauli Kajura kuendesha shughuli zote za kanisa hilo hadi hapo uchaguzi utakapowachagua viongozi wengine wa kanisa.

Wakati kesi ikendelea mahakamani Mwenyekiti huyo aliyeondolewa madarakani kwa masharti ambaye yameelezwa kuwa yalikiuka katiba ameamua leo kutangaza viongozi atakaosaidiana nao kufanya kazi huku akiacha nafasi ya Makamu mwenyekiti bila kutangaza mbadala wake.

Aidha kutangazwa kwa viongozi wapya hao kumewaacha wakristo wakiwa na sintofahamu kufuatia kanisa hilo jimbo la Mashariki kwa sasa kuwa ndani ya Mpasuko kwani baadhi ya wakristo wanaungana na Mch Fumbo na wengine wapo upande wa Kajura.

Fumbo alitangaza kuwa kwa sasa wakati kamati yake inaendelea kujipanga ofisi zitaendelea kuwepo katika ushirika wa Tabata, ikiziacha ofisi za jimbo zilizopo eneo la Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam.

Baadhi wa waumini walipongeza hatua hiyo ya Fumbo huku wengine wakilaani kwa kusema si njia halali ya kutatua migogoro.

No comments:

Post a Comment