Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akiwaonyesha
waandishi wa habari madawa ya kulevya aina ya bangi ambayo yalikamatwa na jeshi
hilo tarehe
07/02/2013.
Askari Polisi wakiwa
wanashusha magunia ya bangi ambayo yalikuwa yanasafirishwa kutoka Arusha
kuelekea Dar es salaam kwa gari aina ya Fuso lenye
namba za usajili T
282 AAJ
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la
Polisi Arusha
Jeshi la Polisi mkoani hapa
limemkamata mtu mmoja akiwa na magunia 97 ya madawa ya kulevya aina ya bangi
ambayo yalikuwa yanasafirishwa toka mkoani hapa kuelekea Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha
Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas amesema kwamba, tukio hilo lilitokea muda wa saa 10:00 alfajiri eneo la Usa River
wilayani Arumeru.
Alisema mafanikio hayo yametokana
na ushirikiano mzuri kati ya jeshi hilo na
wananchi ambapo taarifa za tukio hilo zilitolewa
na raia wema ambapo askari wa jeshi hilo waliweka
mtego eneo hilo
na kufanikiwa kulikamata gari aina ya Fuso lenye namba za
usajili T. 282 AAJ.
Kamanda Sabas aliongeza kwa
kusema kwamba, ndani ya bodi ya gari hilo
kulikuwa na mboga aina ya kabeji iliyosambazwa vizuri huku chini ya mboga hiyo
kukiwa na madawa hayo yaliyokuwa kwenye magunia huku yakivingirishwa kwenye
mifuko ya “plastiki” kwa ndani.
Alisema katika gari hilo kulikuwa na watu
watatu na mara baada ya askari hao kulisimamisha dereva pamoja na msaidizi wake
walifanikiwa kukimbia huku mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Praygod Marick
(22) Mkazi wa Dar esalaam akikamatwa.
Jeshi la Polisi Mkoani hapa
linaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo huku watuhumiwa wengine wakiendelea
kutafutwa. Kwa mara nyingine tena Kamanda huyo aliendelea kuwashukuru wananchi wa Mkoa huu
kutokana na ushirikiano wao mkubwa wanaoutoa kwa jeshi hilo
na kuendelea kuwasisitizia kuimarisha mahusiano na jeshi hilo.
Kwa muda wa kipindi cha mwezi
mmoja toka Januari 07, 2013 mpaka hivi leo jeshi hilo limeshakamata madawa ya kulevya aina ya
mirungi magunia 372 katika magari mawili tofauti na pia limeshakamata jumla ya
magunia 117 ya madawa ya kulevya aina ya bangi ambapo mwanzoni mwa wiki hii jumla
ya magunia 20 yalikamatwa yakiwa yanasafirishwa kwa kutumia wanyama aina ya
Punda maeneo ya Losoiti Wilayani Longido.
No comments:
Post a Comment