Joseph Ngilisho,Arusha
WANAWAKE wawili wanandugu
wameuawa kinyama katika nyumba waliokuwa wakiishi na watu wasiojulikana na
miili yao
kukutwa baada ya siku tatu ikiwa imelaliana huku ikiwa
imeharibika vibaya.
Kugundulika kwa miili hiyo
kumetokea leo majira ya saa 3.15 katika eneo la daraja mbili manipsaa ya
jiji ya Arusha baada ya majirani kuhisi harufu kali iliyokuwa
ikitokea ndani ya chumba hicho walichokuwa wamepanga katika
nyumba inayomilikiwa na merehemu Samson Kivuyo.
Taarifa zimeeleza kuwa majirani
hao walijikusanya na kutoa taarifa kwa uongozi wa eneo hilo ambao kwa pamoja
walikubaliana kutoa taarifa polisi ambapo ,polisi walifika
eneo la tukio na kuvunja mlango,ndipo
walipokuta miili ya marehemu hao
ikiwa imeharibika vibaya.
Miiili ya marehemu hao ilikutwa
na majeraha sehemu mbalimbali za mwili, huku ndani ya chumba hicho
kukiwa kimevurugika na baadhi ya vitu kuvunjika hali ambayo
inaaminika kwamba kabla ya mauaji hayo
kulikuwa na mvutano wa kutoelewana.
Akizungumza na vyombo vya habari
msimamizi wa nyumba hiyo,Fatina Mringo aliwataja marehemu hao
kuwa ni,Zainabu Iddy(Zai) mwenye umri wa miaka 19 na Zena Sadick Shengwatu
mwenye umri wa miaka 40 ambaye alikuwa mfanyabiashara wa nguo na
mmiliki wa chumba hicho.
Alieleza kuwa siku ya jumamosi
marehemu hao walionekana majira ya mchana wakiwa nyumbani, na
marehemu Zena alikabidhiwa fedha na wapangaji wenzake na kwenda
kulipia bili ya umeme Tanesco na baadae alirudi na kuendelea na shughuli
zake kama kawaida.
Hata hivyo habari zimedai kwamba
marehemu hao kwa pamoja hawakuweza kuonekana tena hadi miili yao ilipokutwa chumbani
ikiwa imeharibika vibaya na kutoa harufu kali.
Hata hivyo baadhi ya majirani wakielezea
tukio hilo
wamebainisha kwamba marehemu hao mara nyingi
walionekana kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume tofauti na
kwamba siku ya tukio Zena alionekana akichukuliwa na gari dogo aina ya
teksi huku gari jingine lilionekana likingia nyumbani kwake.
Majirani hao wamedai kwamba
marehemu hao ambao ni wakazi wa Lushoto mkoani Tanga waliishi katika
nyumba hiyo katika mazingira ya kutokuwa na waume .
Kamanda wa polisi mkoani Arusha
Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba uchunguzi unaendelea
na kwamba hadi sasa hakuna aliyekamatwa
kuhusiana na tukio hilo
na miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali
ya mkoa Mount Meru kwa uchunguzi wa daktari.
No comments:
Post a Comment