Raisi Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi kwa furaha isiyo na kifani. |
Kigwangalla alimweleza Rais Kikwete kuwa wananchi wa Nzega wana kipindi cha miaka mitano wanatumia maji machafu kama maji ya kunywa huku uwezekano wa kupata maji safi na salama ukiwapo kwa kiwango kikubwa.
KATIKA hali isiyo ya kawaida jana Wabunge wa Wilaya ya Nzega, Dk Hamis Kigwangalla (Nzega) na Suleimani Zedi wa Jimbo La Bukene walimwambia Rais Jakaya Kikwete kuondoka na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kutokana na kukataliwa na Baraza la Madiwani.
Akizungumza katika kikao cha ziara ya Rais Kikwete, Dk Kigwangalla alisema kuwa mkurugenzi huyo hatakiwi katika halmashauri hiyo kutokana na kutumia miaka mitano kuwanywesha maji machafu wananchi .
Kigwangalla alimweleza Rais Kikwete kuwa wananchi wa Nzega wana kipindi cha miaka mitano wanatumia maji machafu kama maji ya kunywa huku uwezekano wa kupata maji safi na salama ukiwapo kwa kiwango kikubwa.
Alisema Baraza la Madiwani lilishapitisha azimio la kumkataa katika vikao vyake lakini utekelezaji haujafanyika hali ambayo wananchi wanaendelea kuumizwa na suala hilo huku wakiendelea kupata maji machafu kwa matumizi yote ikiwamo kunywa na matumizi mengine. Wakati huohuo, Mbunge wa Jimbo la Bukene Zedi alipopewa fursa ya kuwasalimia wananchi alimuunga mkono mbunge mwenzake kwa kudai kuwa Mkurugenzi mtendaji aondoke kutokana na changamoto mbalimbali ambazo zilielezwa na Mbunge wa Nzega Dk Kigwangalla.
Alisema mambo hayo yalisababishwa na mhandisi wa maji, Mariam Majara kutokana na kushindwa kutekeleza hilo na ni busara kwa Rais kuondoka na viongozi hao wawili.
Jumanne Maghembe, Waziri wa Maji aliposikia suala hilo aliwaahidi wananchi hao kuwa mhandisi wa maji Wilaya, Mariam Majara ataondoka naye katika ziara hiyo ili kuleta ufanisi katika utendajikazi na wananchi hao waweze kupata fursa ya kupata maji safi na salama.Rais Kikwete akiwahutubia wananchi hao alisema kuwa tatizo la maji limekuwa sugu wilayani humo kutokana na uzembe wa utekelezaji wa baadhi ya watumishi ambao umechangia wananchi kutumia maji machafu yenye harufu mbaya.
Alisema halmashauri zinatengewa fedha nyingi za maendeleo kwa lengo la kuwasaidia wananchi ili wasipate shida, lakini imekuwa ni tofauti na malengo hayo kwa jinsi alivyokuwa akitarajia.
Akijibu maombi ya wabunge hao ya kuondoka na mkurugenzi mtendaji pamoja na mhandisi wa maji, Rais Kikwete alisema kuwa suala hilo litatatuliwa na wananchi hao wataendelea na shughuli zao za maendeleo kama hapo awali.

No comments:
Post a Comment