Thursday, January 10, 2013

Makabila yauana tena Mto Tana - KENYA


Mmoja wa waathirika wa mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono kwenye eneo la Kambi ya Wakimbizi wa Somalia ya Daadab,iliyopo Mashariki mwa Kenya Ijumaa iliyopita ambapo watu kadhaa walipoteza maisha na wengine walijeruhiwa.  

Na Mwandishi Wetu, Nairobi
Posted  Alhamisi,Januari10  2013 
 
Kwa ufupi
‘’Inasikitisha kwamba hayo  mauaji yanatokea tena katika kata wakati polisi ndiyo wenye mamlaka ya kuleta amani kushindwa kufanya hivyo wakati polisi kwamba waliokuwa na  mamlaka ya kuleta amani kushindwa kufanya hivyo,”

 ZIKIWA zimebakia siku 53  kufanyika  Uchaguzi Mkuu nchini Kenya hatimaye mauaji mengine yametokea tena Mto Tana uliopo Kaskazini mwa Ukanda wa Pwani nchini Kenya

Mfululizo wa mauaji hayo yaliendelea kutokea jana usiku ambapo watu nane walipoteza maisha huku wengine kadhaa wakijeruhiwa ,katika vijiji vya Nduru baada ya kabila la Orma kulikabili kabila la Pokomo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa kata hiyo ya  Mto  Tana Gure Golo, alisema kwamba wavamiaji waliingia majira ya usiku wa saa tano katika kijiji  hicho ambapo waliua watu na kuwaumiza wengine.
‘’Inasikitisha kwamba hayo  mauaji yanatokea tena katika kata wakati polisi ndiyo wenye mamlaka ya kuleta amani kushindwa kufanya hivyo wakati polisi kwamba waliokuwa na  mamlaka ya kuleta amani kushindwa kufanya hivyo,” alisema

Aliongeza kwamba kwa sasa wanahofia maisha yao kuwa hatarini kutokana na Jeshi la Polisi kushindwa kuweka ulinzi wa kutosha katika eneo hilo jambo ambalo wakazi wengi wameshaondoka kwa kuhofia maisha yao.

Naye mkuu wa polisi wa eneo hilo Tana Richard Mukwate alithibitisha  kutokea kwa mashambulizi hayo na kukiri kuuawa kwa watu hao huku wengine wakiwa majeruhi.
Waliojeruhiwa kwa mapanga na risasi walikimbizwa katika Hospitali ya Malindi Wilaya na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya..

Mwaka jana mapigano hayo yalizuka katika eneo hilo , ambako hadi kufikia sasa watu 39 walilipotiwa kufariki, ikiwa ni miezi michache tu baada ya ghasia nyingine kuua watu 100.

Wengi ni wanawake na watoto
Maofisa wa Msalaba Mwekundu nchini Kenya walisema kuwa wengi walipoteza maisha yao katika mazingira hayo ya kuvuja damu kupita kiasi baada ya kukosa matibabu ya dharura.
Miongoni mwa waliouawa wakati wa mashambulizi hayo ni watoto 13, wanawake sita wanaume 11 pamoja na wavamizi tisa.

Hata hivyo maofisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya walisema kuwa idadi hii huenda ikaongezeka kwani juhudi za kuwatafuta majeruhi waliotorokea vichakani bado inaendelea.
Hospitali kuu ya wilaya ya Malindi ilikuwa na shughuli nyingi kwa wakati mmoja na kuonekana kushindwa kukabiliana na idadi ya marejuhi.

Mauaji haya yanatokea hatua chache tu kutoka eneo la Kilelengwani ambako zaidi ya watu 100, mifugo 400 na nyumba kuchomwa moto mwezi Agosti mwaka jana.
Wenyeji wa eneo hilo wanainyoshea kidole Serikali na viongozi wa siasa kwa kile wanachokitaja kuwa mauaji ya halaiki.

Bado ya Agosti hayajasuluhishwa
Kutokana na mauaji ya mwezi Agosti, Serikali ya Rais Mwai Kibaki ilipeleka vikosi vya Jeshi la Polisi na kutangaza amri ya kutokutoka nje katika eneo hilo ambayo wenyeji wanasema kuwa ilidumishwa kwa muda mfupi.

Aidha Serikali ya Rais Mwai Kibaki pia ikateua tume ya kuchunguza mauaji hayo ya mwezi Agosti ikiongozwa na Jaji Grace Nzoika kuhusiana na mauaji hayo ya Tana River.

Awali Jeshi la Polisi nchini Kenya liliwataka wale wote ambao wanamiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha mara moja kabla ya kuanza mchakato ikiwa ni sehemu ya kuimarisha usalama nchini humo.Baada ya tukio hilo polisi walitangaza kuwakamata watuhumiwa zaidi ya 60 waliohusika na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment