Saturday, January 5, 2013

Miradi 4 ya barabara kuzinduliwa Tabora

Written by  Mwandishi wetu

Ujenzi wa barabara ukiendeleaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa miradi ya barabara na daraja katika mkoa wa Tabora kuanzia tarehe 7 Januari 2013.

Pamoja na shughuli nyingine, Jumatatu tarehe 7 Januari 2013 akiwa mkoani humo,Mhe. Rais kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa ujenzi wa Daraja la Mbutuliloko Wilayani Igunga.Jumanne tarehe 8 Januari 2013, Mhe.

Rais ataweka jiwe la msingi la uzinduzi waujenzi kwa lami wa barabarai)

Siku ya Jumatano ya tarehe 9 Januari 2013 Mheshimiwa Rais ataweka jiwe la msingila ujenzi wa barabara ya Ndono hadi Urambo.

Uzinduzi wa miradi hii ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuhakikishakuwa Makao Makuu ya Mikoa yote yanaunganishwa kwa barabara za lami.

Miradihii ni mafanikio makubwa katika sekta ya usafirishaji na itatoa chachu kubwa kwauchumi wa mkoa wa Tabora na Taifa kwa ujumla.

Aidha, miradi hii itasaidia sanakatika kuimarisha Usafiri wa barabara kati ya Tabora na mikoa ya Kigoma,Shinyanga, Singida na Dodoma.

MUENDELEZO WA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM YA 2010

No comments:

Post a Comment