
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga makofi mara
baada ya kumkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi
anayenyanyua juu juu tuzo ya Mbuga ya wanyama ya Serengeti mara baada ya
kuitangaza mbuga hiyo kuwa ni moja ya maajabu saba ya asili katika bara la
Afrika kwenye hoteli ya Mount Meru, Kushoto ni Bw Philip Imler Mwanzilishi wa
Taasisi ya Seven Natural Wonders
Bw. Philip Imler.
Tanzania imefanikiwa kushinda kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crates na Mbuga ya wanyama ya Serengeti, hafla hiyo imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabalozi, Wafanya biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na wadau mbalimbali wa utalii kutoka Mataifa mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki
Katika picha kulia
ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na Lynn Imler mmja wa
wakurugenzi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi
ya picha ya Ngorongoro Crates
muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders
Bw.Phillip Imler mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu saba
ya asili ya Afrika iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini
Arusha.

Vikundi wa ngoma kutoka makabila ya mkoa wa
Arusha vilipamba hafla hiyo kamavinavyoonekana

Wadau kutoka TTB ambao pia walikuwa ni
miongoni mwa wanakamati ya maandalizi wakiwa
katika picha ya pamoja

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Dk. Aloyce
Nzuki akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini Mchungaji Msigwa, Kushoto
ni Mh Shah kutoka Mafia na mmoja wa wajumbe wa bodi ya Utalii TTB

Wabunge wa bunge la
Jamhuri ya Muungano ya Tanzaniaakiwa katika hafla hiyo.

Viongozi mbalimbali
wa dini walihudhuria pia.

Mbunge Mh. James Lembeli akisalimiana na Bw.
Mike Teylor walipokutana katika hafla hiyo.

Mwanamuziki Mrisho Mpoto na Kundi lake wakitumbuiza
wakati wa utoaji wa tuzo hizo.

Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Bi
Devitha Mdachi akiwa pamoja na maafisa wengine wa bodi hiyo wakipokea wageni
mbalimbali waliofika katika hafla hiyo.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis
Kagasheki akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk.
Aloyce Nzuki.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis
Kagasheki akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Maimuna Tarishi
katikati ni msaidizi wake Bw. Miskanji.

Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika hafla
hiyo.

Waziri Mkuu akiwa meza kuu pamoja na viongozi
wengine wakati wa utoaji wa tuzo hizo za Seven Natural Wonders jijini Arusha
jana jioni., kutoka kulia ni Magesa Mulongo mkuu wa Mkoa wa Arusha, Agness
Agunyu Waziri wa Utalii kutoka nchini Uganda na kutoka kushoto ni Bw. Philip
Imler kutoka Taasisi ya Seven Natural Wonders na Waziri wa Maliasili na Utalii
Balozi Khamis Kagasheki.

Mkurugenzi wa Hifadhi za taifa TANAPA Bw.
Allan Kijazi akiwasikiliza wabunge waliohudhuria katika hafla hiyo kulia ni Deo
Filikunjombe na kushoto ni David Kafulila.

Waziri Mkuu Mizengo
Pinda akiongozwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki wakati
alipowasili kwenye hoteli ya Maount Meru kwa ajili ya utoaji tuzo hizo.

Mama Tunu Pinda wa
pili kutoka kushoto akiwa katika hafla hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya
Utalii Tanzania (TTB) Dk Aloyce Nzuki na katikati ni Lynn Imler kutoka Seven
Natural Wonders.

Mabalozi mbalimbali
waliohudhuria katika hafla hiyo wa kwanza kutoka kulia ni Balozi Mutinda Mutiso
Balozi wa Kenya Nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa Bodi ya
Utalii nchini Tanzania (TTB) Dk. Aloyce
Nzuki akiongea katika hafla hiyo.

Bw Allan Kijazi kushpto akiwa na wadau wengine katika hafla
hiyo.

Waziri Mkuu Mizengo
Pinda akimkabidhi tuzo ya Hifadhi ya Ngorongoro Crates Mkurugenzi wa Hifadhi za
Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi katika
hafla hiyo, kushoto ni Philip Imler wa Seven Natural Wonders.

Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi
akiongea katika hafla hiyo.

Muanzilishi na
muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler akizungumza
katika hafla hiyo.

Tuzo ya mlima
Kilimanjaro ikapokelewa na mhifadhi wa mlima huo kulia ni Waziri Mkuu Mizengo
Pinda na Philip Imler kushoto.

Balozi Khamis
Kagasheki ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii akizungumza katika hafla
hiyo iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.

Waziri Mkuu Mizengo
Pinda akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount
Meru jijini Arusha.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania akizungumza na Balozi
Charles Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB na Mkurugenzi wa
bodi hiyo Dk. Aloyce Nzuki wakati wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment