
PADRI EVERIST MUSHI (PICHANI) WA KANISA KATOLIKI
HUKO ZANZIBAR,AMEPIGWA RISASI YA KICHWA NA WATU WASIOJULIKANA NA KUFARIKI PAPO
HAPO ASUBUHI HII WAKATI AKIELEKEA KWENYE IBADA KATIKA KANISA LA MTONI,ZANZIBAR.
SABABU ZA KUPIGWA RISASI KWA PADRI HUYO BADO HAZIJAFAHAMIKA
MPAKA SASA.
MASHUHUDA WA TUKIO HILO WANASEMA KUWA WATU HAO WALIOFANYA
TUKIO HILO WALIKUWA NI WAWILI NA WALIKUWA WAMEPAKIZANA KWENYE PIKIPIKI AINA YA
VESPA WAKATI PADRI HUYO ALIKUWA KWENYE GARI LAKE AMBALO BAADA YA KUTOKEA KWA
TUKIO HILO NALO LILIACHA NJIA NA KWENDA KUGONGA NYUMBA MOJA ILIYOKUWA JIRANI NA
KANISA HILO.
No comments:
Post a Comment