
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akivuta waya kuashiria kufyatua mtego wa kuwasha moto wa
kuteketeza Silaha haramu, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika zoezi hilo la
uteketezaji wa silaha haramu, Lililofanyika katika Kambi ya Magereza jijini Dar
es Salaam, Jumamosi Feb 16, 2013. Kushoto kwake ni Kamishna msaidizi wa Jeshi
la Polisi Tanzania, Simon Siro na wa pili kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani, Perera Ame Silima na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kmataifa, Benard Membe.

Sehemu ya Silaha hizo zikianza kuteketea kwa moto baada ya
Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufyatua waya maalumu wa kuwasha
moto huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi, baada ya kusimamia zaoezi la
uteketezaji wa Silaha haramu, lililofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi,
Simon Siro, wakati wakipita kukagua sihala hizo haramu kabla ya kuanza kwa
zoezi la uteketezaji wa silaha hizo haramu lililofanyika Ukonga jijini Dar es
Salaam.

Silaha haramu zilizoteketezwa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma
hotuba yake wakati wa zoezi la uteketezaji wa Silaha Haramu, lililofanyika
Ukonga Jijini Dar es Salaam.

Wimbo wa Taifa, kabla ya kuanza kwa zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment