Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.
Bernard K. Membe (Mb.), akiweka saini Itifaki ya Amani na Usalama ya Nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Uwekaji saini huo ulifanyika katika Hoteli
ya New Africa, jijini Dar es Salaam.
Mhe. Membe (wa pili kushoto) akiwa na viongozi wenzake wa
nchi za EAC wakiwa wameshikilia Itifaki hiyo mara baada ya kusainiwa
Mhe. Membe akipitia Itifaki hiyo kabla ya kusainiwa huku Bw.
John M. Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa akishuhudia.
Mhe. Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wake Bw. Haule.
Mwingine katika picha ni Mhe. Pereira Ame Silima (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Picha nyingine ya Mhe. Membe na Katibu Mkuu wake Bw. Haule
na wajumbe wengine waliohudhuria mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard
Sezibera (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Ulinzi wa Uganda.
Mhe. Membe akifanya mahojiano na Waandishi wa Habari baada
ya shughuli ya utiaji saini kukamilika.
Picha zaidi za mahojiano kati ya Mhe. Membe na Waandishi wa
Habari.
No comments:
Post a Comment