Monday, February 4, 2013

KUTOKA BUNGENI LEO

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Job Ndugai akitoa miongozo mbalimbali Bungeni leo.
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella Mukangara akifafanua hoja ya Serikali ya Mfuko wa Mikopo kwa Vijana leo Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge wa Ubungo,Mh. John Myika akiwasilisha hoja binafsi juu ya kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika jiji la Dar es salaam Bungeni leo.
Wabunge wa upinzani wakiwa wamesimama wote kwa pamoja kupinga
hoja leo Bungeni.
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Tundu Lissu akitoka
 ndani ya ukumbi wa Bunge leo.
Naibu Spika Bunge,Mh. Job Ndugai (kulia) akionyeshwa makabrasha na
Mbunge wa Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari muda mfupi
 baada ya kuahurishwa kwa kikao cha Bunge leo.
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Tundu Lissu (kulia} akijadiliana jambo na Naibu Spika wa Bunge,Mh. Job Ndugai nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari na Mbunge wa Iringa Mjini,Mchungaji Msigwa.
Baadhi ya wabunge wakielekea ndani ya ukumbi wa Bunge leo Dodoma.
Picha na Mwanakombo Jumaa,Maelezo.

No comments:

Post a Comment