Written by
Mwandishi wetu
Mkurugenzi Mkuu wa Palace Hoteli Arusha, Fred Maina akizungumza na Mwandishi wa Habarimpya.com,hayupo pichani Arusha
JIJI la Arusha imefanikiwa katika suala la Utalii na Uwekezaji huku
ikikabiliwa na Changamoto za usafi . Jiji hilo limeweza kupiga hatua
zaidi na kutambulika vyema Afrika Mashariki na Kati lakini mamlaka
zinazohusika zimeshindwa kutatua changamoto za usafi.
Katika sekta ya uwekezaji jiji la Arusha linapambwa na hoteli nyingi
zenye hadhi ya nyota tano na moja ya Hoteli nzuri na za kisasa ni Palence
Hoteli Arusha iliyopiga hatua kubwa katika kipindi cha miezi 11 tangu
kuanzishwa kwake.
Watu mbalimbali wakiwa wamepumzika katika bustani ya Jiji la Arusha inayotunzwa na Palace Hoteli Arusha.Akizungumza na Habarimpya.com
hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli hiyo Fred Maina anasema kwamba
mbali na kuzingatia ubora wa vyakula, malazi huduma nzuri kwa wageni pia
wamefanikiwa katika suala la kuhifadhi mazingira baada ya kutengeneza
miundombinu mizuri ya maji taka na kuboresha mazingira ya nje ya Hoteli.
“Tumeamua kuiboresha bustani iliyoko mbele ya Hoteli yetu na kuwa
kivutio kikubwa kwa wakazi wa Jiji la Arusha eneo hilo limekuwa kivutio
kikubwa kwa waandaaji wa sherehe ya kipaimara, harusi kuja kupiga picha
za kumbukumbu nani sehemu nzuri ya kupumzikia nyakati za mchana na
usiku”anasema Maina.
Hii ndiyo maegesho ya magari yanayolindwa wa Askari wa Palace Hoteli Arusha.Picha zote na Jackson OdoyoMbali
na Bustani hiyo,Palace Hoteli imefanya maboresho makubwa ya maegesho ya
magari katika eneo la bustani hiyo yenye ulinzi na usalama wakutosha.
Palace Hoteli Arushai iko katikati ya Jiji, inamalengo makubwa ya
kuhakikisha wageni wote wanaofika katika Jiji hilo kwa shuguli
mbalimbali za kikazi,biashara na mikutano wanapata huduma safi ya malazi
na vyakula kwa bei nafuu.
Hoteli hiyo iko karibu na Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa (AICC),Makao Makuu ya Afrika ya Mashariki na Kati,(EAC).
Wakati Palace Hoteli Arusha ikijivuna kuwa rafiki wa mazingira, jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Dk. Terezya Huvisa mwaka jana mwishoni aliifunga Hotel ya Double Tree kwa kushindwa kutunza mazingira.
No comments:
Post a Comment