Monday, January 28, 2013

LULU APATA DHAMANA LEO MAHAKAMA KUU JIJINI DAR

 Msanii Elizabeth Michael (Lulu) akizungumza na wakili wake peter Kibatala muda mfupi kabla ya kuanza kusikilizwa ombi lake la dhamana leo asubuhi kwenye Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam,ambapo dhamana imepatikana kwa masharti mashahidi wawili wafanyakazi wa Serikali kwa bondi ya
 Tsh 20 Milioni kila mmoja na masharti mengine tumeorodhesha kwenye habari hapo chini.
 Msanii Elizabeth Michael (Lulu) akiwasili kwenye kizimba cha Mahakama Kuu leo Jijini Dar es Salaam.
 Msanii Elizabeth Michael (Lulu) (katikati) akisubiri kusikiliza maombi yake ya dhamana kusomwa na
 Jaji anayesikiliza kesi hiyo Mhe. Zainabu Mruke leo Jijini Dar es Salaam.
 Ndugu jamaa na marafiki wa msanii huyo na baadhi ya watu wengine wakiwa kwenye chumba 
cha Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam wakisubiri kusikiliza maombi ya dhamana.
 Wakili wa lulu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mteja 
wake kupatiwa dhamana.
Msanii Muhusin Awadi (Dr.cheni) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya 
kutolewa dhamana ya msanii huyo.

Hatimaye Msanii wa Filamu nhini Elizaberth mhael maarufu kwa jina la Lulu, mchana wa leo amepata dhamana na kuachiliwa kutokana na kesi inayo mkabili ya kuua bila kukusudia msanii mwenzake wa filamu marehemu Steven Kanumba mwaka jana.

Akisoma masharti ya dhamana Jaji anaesikiliza kesi hiyo Zainabu Mruke, alitaja masharti kadhaa ambayo mtuhumiwa atatakiwa kuyatekeleza kabla ya kupewa dhamana hiyo.

Mruke alisema mtuhumiwa atatakiwa kuwasilisha hati zake za kusafiria zote mahakamani hapo, atatakiwa kuwa na wadhamini wawili wafanyakazi wa Serikali ambao kila mmoja atatatkiwa kuweka udhamini wa Tsh 20 Milioni kama bondi na sio fedha taslimu.

Aidha Jaji mliongeza kuwa mtuhumiwa hataruhusiwa kusafiri nnje ya Jiji la Dar es Salaam isipokuwa kwa ruhusa maalum ya Mahakama.

Wakili wa mshitakiwa huyo Peter Kibatala alisema amefurahishwa na dhamana aliyopatiwa mteja wake na wataendelea na kazi ya kumtetea hadi mwisho wa kesi hiyo.

Wasanii wenzake waliojitokeza na kuonekana Mahakamani hapo ni pamoja na 
Muhsin Awadh (Dr. Cheni) na Steve Nyerere. Akizungumza na 
waandishi wa habari mara baada ya hukumu hiyo Dk. Cheni alisema yeye binafsi
 amefurahishwa na dhamana hiyo na yuko tayari kufanya naye kazi.

No comments:

Post a Comment