Tuesday, February 19, 2013

Ziara ya Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo mkoani Arusha

 
 Waziri wa  Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Mh. Dkt. Fenella Mukangara (mwenye miwani ) leo amepokea taarifa ya kikundi cha Petu Saccos na kuongea na  vijana wa kikundi cha Youth Welding Group cha Sanawari  - Arusha (pichani) alipotembelea na kuangalia jinsi fedha za mfuko wa vijana zilizotolewa  wizara yake zilivyowanufaishavijana katika kujikomboa kimaisha na kujiajiri wenyewe.
 
 Waziri  wa Habari , Vijana, Utamaduni na Michezo  Mh. Dkt.Fenella Mukangara (alivaa miwani ) akiongea na wana Saccos wa Petu kupitia kikundi cha Youth Welding group cha Sanawari  mkoani Arusha leo
 
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na .  Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kushoto)leo akizungumza na Mjasiriamali Martha  Yusuph alipotembelea  Soko kuu Saccos Arusha na kuangalia wanufaika wa mikopo ya mfuko wa vijana uliotolewa na Wizara yake
 
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mjasiriamali wa  Krokon Saccos Asha Muhamed jinsi alivyonufaika  mkopo wa mfuko wa Vijana kutoka Wizara yake .
 
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Mh. Dkt. Fenella Mukangara (alievaa miwani) akiongea na wafanyakazi wa  TBC na Mafundi wa Star Times leo alipotembelea  Njiro mkoani Arusha  kuangalia shughuli mbalimbali. Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO

No comments:

Post a Comment