Sunday, May 5, 2013

Mlipuko Watokea Katikati ya Ibada na Kujeruhi Katika Kanisa Katoliki Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mulongo akiteta jambo na mmojawapo wa viongozi wa Usalama - Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh. Magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na wananchi kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa. Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi. Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea
Ulinzi ukiwa umeimarishwa Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi. Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Mh Gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.

No comments:

Post a Comment