Saturday, January 5, 2013

Zitto:Sitasema kitu kuhusu Urais 2015

Written by  Mwandishi wetu

Zitto Kabwe         Dar es Salaam
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ameelezea hisia zake kuhusu uchaguzi wa rais  mwaka 2015 na kudai kuwa kwa sasa hata kuwa tayari kuongelea suala hilo hadi hapo katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania itakapokamilika.

Wachambuzi na wadadisi wa mambo ya siasa wanaelezea kuwa msimamo huo wa Zitto Kabwe ni kufungwa mdomo, na ni matokeo ya kikao chao cha siku kadhaa kilichokaaa kwa ajili ya kujadili mstakabali wa chama hicho katika uchaguzi ujao


Akielezea hoja hii kwenye ukurasa wake wa FB zito alisema " Ngoja niweke wazi kabisa. Ninaulizwa sana kuhusu suala la Urais 2015 baada ya kauli za wanachama waandamizi wa CHADEMA kunukuliwa kuzungumzia suala hilo:

Aliongeza kuwa Jibu langu kwa wote wenye kutaka kusikia kauli yangu ni kwamba 'katika moja ya maazimio yangu ya mwaka mpya 2013 ni kutoongelea kabisa suala la Urais 2015.

"Hivyo sitaongelea suala hili. Sitasema kitu kuhusu suala hili mpaka baada ya Katiba mpya kupatikana na chama changu kuweka utaratibu na mchakato wake,"alisema Zitto kabwe.
 Endelea kuwa nasi kwa habari zaidi

No comments:

Post a Comment