by Pamela Mollel
Viongozi wa Dini (Wachungaji) wakifanya maombi ya mwisho
kabla ya kuuhifadhi mwili wa aliyekuwa Mjumbe
wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), ngazi
ya Taifa kupitia Mkoa wa Arusha, Benson
Mollel (26) aliyeaga dunia hivi karibu
Baadhi ya Viongozi walio hudhuria mazishi ya Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha
Mapinduzi (UVCCM), ngazi ya taifa
kupitia mkoa wa Arusha, Benson Mollel (26) aliyeaga dunia hivi karibu
katika hoteli ya Lush Garden Bussines Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala
na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la
Arusha
Mama Mzazi wa Marehemu Benson Mollel akiwa analia kwa uchungu
baada ya kuweka shada la maua juu ya kaburi la mwanaye
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas
akiwa anatoa heshima za mwisho mara baada ya kuweka shada la maua
Naibu waziri wa nishati na madini Steven Masele katikati
aliye valia nguo ya kijani na miwani akishuudia mazishi ya Benson Mollel
Mfanya biashara wa madini maarufu jijini Arusha Bw. Mathias
Manga akiwa na Mkewe wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Benson
Mollel
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli Mh.Edward
Lowassa akiwa amebeba shada la mau kabla ya kuweka kaburini.
Maelfu ya wananchi wakiwemo viongozi mbalimbali wa kitaifa,
viongozi wa dini, vyama vya siasa walijitokeza kumzika aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha
Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia
mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyeaga dunia hivi karibu katika hoteli ya
Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda
mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.
Viongozi walioudhuria msiba huo jana nyumbani kwa marehemu
katika kata ya Lemara jijini Arusha ni pamoja na Waziri mkuu mstaafu na mbunge
wa jimbo la Monduli Mh.Edward Lowassa, Naibu waziri wa ardhi nyumba na makazi
Godluck Ole medeye, Naibu waziri wa nishati na madini Steven Masele, Mkuu wa
mkoa wa Arusha Magesa Mulongo, Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo
pamoja na viongozi mbalimbali wa UVCCM Taifa na Mkoa.
Msiba huo ulikuwa wa aina yake kutokana msururu wa magari
pamoja na umati mkubwa wa watu kufika hali iliyopelekea
wananchi wengine kushindwa hata kuaga
mwili wa marehem kutokana na ufinyu wa eneo hilo
Katika salamu za rambirambi Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa
Arusha Robinson Meitenyiku alisema kuwa marehemu ameacha pengo kubwa sana kwana
UVCCM na hata kwa wananchi huku akiwataka vijana kumrudia Mungu kutokana na
vijana wengi kufa kwa umri mdogo hali ambayo inapelekea nguvu kazi ya taifa
kupungua.
“Benson alikuwa mjumbe wa baraza mkoa,kamati ya utekelezaji
mkoa na mjumbe wa baraza Taifa tunajua alikuwa na malengo gani na ndiyo
tutaenda kuyafanya kwasababu alikuwa ni kiongozi mpenda maendeleo katika
jamii”Alisema Meitenyiku
Hata hivyo aliweka wazi kwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa
Tanzania Jakaya Kikwete kuwa toka aingie madarakani pamoja na marehemu
hakujawahi kuwepo na makundi katika UVCCM mkoa wa Arusha
“Tunamshukuru Rais kwa salamu zake ila ajue kuwa toka
Robinson na Benson waingie madarakani hatujawahi kuwa na makundi ya aina yeyote
ile hivyo ushindi uko pale pale”alibainisha
Meitenyiku
Kwa upande wake Naibu waziri wa ardhi nyumba na makazi
Goodluck ole Medeye aliwataka vijina kutokukata tama pamoja na kuzingatia elimu
inayotolewa na viongozi wa dini,serikali ili kuepuka uvunjifu wa amani hapa nchini.
“Marehemu alikuwa ni mfano mzuri wa kuigwa kutokana na
alipenda amani…..Nilipopata taarifa kuwa Benson amefariki nilijiwa na picha ya
mgomba mchanga uliyochipua ulipokaribia kuchanua ukakatwa ghafla …..matunda
ambayo tulitarajia kuyapata katika mgomba huo hatujayapata “alisema
Aidha aliwakumbusha vijana mshikamano pamoja na upendo
miongoni mwao huku akiwataka watumie ujuzi walionao katika kuliendeleza Taifa
na kuondoa umaskini.
No comments:
Post a Comment