Monday, January 7, 2013

NCHI ZA UKANDA WA KUSINI NA AFRIKA MASHARIKI ZIMESHAURIWA KUBUNI NJIA BORA ZA UZALISHAJI WA BIDHAA ILI KUPUNGUZA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

by Mwandishi Wetu 

 Waziri wa viwanda na biashara DK.Abdalah Kigoda akiongea na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi jana jijini Arusha katika mkutano wa siku mbili wa wadau wa mazingira na wazalishaji katika hotel ya Naura.

 Nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini zimeshauriwa kubuni na kuzingatia njia bora za uzalishaji wa bidhaa zake ambazo ni rafiki wa mazingira na zinazo kidhi viwango vya ubora wa kimataifa(TBC)

Akizungumza na waadishi wa habari muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku mbili jana jijini Arusha, yenye lengo la kujadili ni njia zipi zitumike kupunguza athari za uharbifu wa mazingira,Waziri wa Viwanda na Biashara DR.Abdalah Kigoda amesema bado kunahitajika elimu ya kutosha kwa wanaanchi kuelewa juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi

DR.Kigoda alisema  kuwa wazalishaji hawana budi kuweka utaratibu unaofaa ambao utasaidia kupatikana kwa njia bora za uzalishaji kuanzia malighafi,usafirishaji wa malighafi  na zao la mwisho  litokanalo na malighafi hiyo ili kupunguza uharibifu wa mazingira

"Ni utaratibu gani utatumika katika msururu wote huo ili kupunguza uharibifu wa mazingira hiyo itasaidia mazingira kutoharibiwa kwa kiasi kikubwa"alisema Kigoda

Alisema kuwa Swala hili linahitaji elimu kubwa,pamoja na kiwango fulani cha teknolojia kwa kuwa inachukuliwa kuwa ni ushindani katika soko

"Sisi Nchi zilizoendea tunapata changamoto kubwa sana ya kuingiza bidhaa zetu katika soko la dunia kutokana na viwango,masharti mbalimbali,kanuni mbalimbali,eneo hili tuliangalie kwa umakini sana inaweza kuwa kikwazo cha biashara"alisema

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu TBS,Leandri Kinabo aliweza kuishukuru shirika la dunia inayohusika na kuandaa viwango (ISO) kwa kuweza kuandaa mkutano huo ambao umewashirikisha wadau mbalimbali wa mazingira

"Mikutano kama hii hasa yenye kuweka mikakati ya viwango hususani kwenye uzalishaji bora unaozingatia mazingira ni mara chache sana kufanyika katika bara la Afrika,,,safari hii wamechagua Tanzania tunawashukuru sana"alisema Kinabo

Aidha alisema kuwa (ISO) wamepanga mambo makuu mawili ambapo moja ni kufadhili warsha hiyo  TBS ambapo nchi zote za ukanda wa Mashariki ya Afrika ,pamoja na nchi zote za SADEC.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS,Leandri Kinabo akiongea na vyombo vya habari leo jijini Arusha 
Washiriki wa Mkutano wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Waziri Abdalah Kigoda.

No comments:

Post a Comment